Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemsweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects ambaye alitoa taarifa ya uongo kwa Waziri huyo kuhusu ujenzi wa Makao Makuu ya Uhamiaji Mkoani humo.
Tukio hilo limetokea wakati Waziri Lugola na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Meja Jenerali, Jacob Kingu walipofika katika Kituo hicho kikuu cha mkoa kwa kushtukiza wakati alipokua anakwenda Uwanja wa Ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam.
“Hivi ndivyo Polisi mnafanya hivi, haya ndio madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi? RPC hawa polisi wako wanafanya nini, OCS njoo hapa, kwanini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,”amesema Lugola
Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya amemueleza Waziri Lugola kuwa, Polisi wake wamefanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.
-
JNIA yapiga marufuku wagonjwa wa Ebola kuingia nchini
-
Video: Rais Mstaafu Kikwete akwea Pipa kuelekea nchini Zimbabwe
-
Rais Magufuli alivyotembelea shamba la mboga la marehemu dada yake
Kwa upande wake mkuu wa kituo hicho, Ibrahim Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, alisema sababu kuu yakutowaweka mahabusu watuhumiwa hao ni kwasababu mahabusu ilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea mahabusu wamekuwa wengi kituoni hapo.