Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain wanajipanga kumsajili, Joao Felix ili atue katika mji mkuu wa nchi hiyo katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya Kiangazi.

Felix alianza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya akirejea Atletico Madrid juma hili, na katika mkutano na viongozi wa klabu hiyo alithibitisha anataka kuondoka katika klabu hiyo msimu huu wa joto.

Mtandao wa 90min umeeleza kuwa Felix anatamani kuhamia Paris Saint-Germain ili kufanya kazi na kocha mpya, Luis Enrique.

Enrique amewasili Parc des Princes, akichukua nafasi ya Christophe Galtier, na vyanzo vimethibitisha amemtaja Felix kama mchezají anayetarajiwa kusajiliwa na mabingwa hao wa Ligue 1 majira haya ya joto.

Kwa hali ilivyo, Atletico Madrid wanadai takriban euro milioni 90 kwa huduma ya fowadi huyo, wakiwa wamelipa zaidi ya euro milioni 120 kumsajili kutoka Benfica mwaka wa 2019.

Kwa mujibu wa 90min PSG ingependelea mkataba wa mkopo, ikiwa na chaguo la kumnunua, lakini Atletico wanataka kumuuza jumla.

Felix alitumia kipindi cha pili cha msimu uliopita kwa mkopo akiwa Chelsea, mkopo ambao haukujumuisha jukumu la kununua, na klabu ikaamua kutotumia nafasi hiyo kumsajili fowadi huyo wa Ureno moja kwa moja kwa kuwa haendani na mipango ya Mauricio Pochettino pale Stamford Bridge.

Klabu nyingine za England zinazohusishwa na kumwania mchezaji huyo ni pamoja na Manchester United, Tottenham Hotspur, Newcastle United na Aston Villa.

Waliofariki ajali ya Hiace, lori watambuliwa
Fahamu viumbe vitano vinavyokufa baada ya kuzaa