Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris-Saint German Luis Enrique anafikiria kuondoka baada ya siku 30 tangu alipotambulishwa kuwa kocha wa klabu hiyo kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.

Kocha huyo wa zamani wa FC Barcelona amechoshwa na mzozo unaoendelea kati ya Kylian Mbappe na uongozi wa klabu hiyo kuhusu hatima yake baada ya kugoma kusaini mkataba mpya.

Kufuatia sakata hilo klabu ya Al-Hilal ilimuwekea mezani ofa ya Pauni 259 milioni, hata hivyo Mshambuliaji huyo aligoma kuzunguma na mabosi wake.

Kwa mujibu wa ripoti, Mbappe hana mpango wa kukipiga Saudi Arabia kwani bado hajatimiza ndoto zake ikiwemo kubeba ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya.

Aidha mpaka sasa hatima yake bado haieleweki kama atakipiga PSG baada ya kupigwa ‘stop’ na inasemekana klabu hiyo inataka kumuuza hadi dirisha la usajili la kiangazi mwakani ili asiondoke bure.

Mbappe alizuiwa kufanya mazoezi na klabu hiyo baada ya kubainika aliwasiliana na Real Madrid kuhusu uhamisho wake.

Hata hivyo, PSG imepinga taarifa hiyo ikidai ni upuuzi. Chanzo cha habari kimeripoti msemaji wa klabu hiyo alimwambia Fabrizio Romano na kuwataarifu mashabiki wasiwe na hofu kuhusu kocha wao.

Enrique alijiunga na PSG kipindi hiki cha usajili wa kiangazi baada ya kumfukuza Christophe Galtier licha ya kuipa ubingwa wa Ligue.

Tabora United yaanika vyuma hadharani
Bila Dola tutashindwa Kuagiza - Waagizaji wa Mafuta