Uongozi wa Mabingwa wa Soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain unatarajia kumtambulisha Kocha kutoka nchini Hispania, Luis Enrique kuwa Mkuu wa Benchi la Ufundi baada ya timu hiyo kuachana na Christophe Galtier.

PSG wanajipanga kumtambulisha Enrique ambaye alipata mafanikio makubwa akiwa na klabu ya Barcelona ya kwao Hispania, ili kukifundisha kikosi chao ambacho kinahaha kusaka ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ‘UEFA’

Tayari mabosi wa PSG na Enrique wameshakubaliana juu ya mkataba wa miaka miwili ambao kocha huyo atausaini na kuanza kazi ndani ya kikosi hicho ambacho kimekuwa kikimwaga fedha nyingi kwa kila msimu.

Kocha huyo anatarajia kuanza kazi ndani ya timu hiyo wakati wa msimu ujao wa Ligi Kuu Ufaransa ‘Ligue 1’utakapoanza na atakutana na wachezaji wapya Manuel Ugarte, Marco Asensio, Lucas Hernandez, Kang-in Lee, Cher Ndour na Milan Skriniar ambao wapo kwenye mipango ya msimu ujao 2023/24.

TPLB: Tutasimamia kanuni ipasavyo 2023/24
Azam FC, Lusajo Mwaikenda hadi 2025