Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbrazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ kwa sasa anafikiria kuanza kumpa dakika nyingi za kucheza kiungo wake mpya, Luis Miquissone raia wa Msumbiji.

Kiungo huyo ni kati ya wachezaji waliosajiliwa na Simba SC msimu huu ambapo Luis tangu ajiunge na timu hiyo, amekuwa hajawa vizuri kulinganisha na alivyokuwa akicheza hapo awali.

Akizungumza jijini Dar es salaam Robertinho amesema Luis ni mchezaji mzuri mwenye kipaji kikubwa cha kucheza soka, lakini bado anahitaji muda wa kumuandaa ili acheze dakika nyingi ambapo katika michezo ijayo, amepanga kumtumia kwa zaidi ya dakika 40.

Ameongeza kuwa, anafurahia kumuona kiungo huyo akibadilika na kuwa fiti zaidi kadiri siku zinavyokwenda, akiamini kwamba akiendelea kucheza zaidi atakuwa tishio.

“Uwezo wa Luis kwa sasa ni mkubwa na umebadilika tofauti alivyokuja wakati tukiwa kambini Uturiki, alikuja akiwa amekosa mechi fitinesi, lakini sasa anaonekana ana kitu katika timu.

“Tukiwa Uturuki nilikuwa namtumia kucheza dakika 25, na sasa namtumia kwa dakika mpaka 40, sio rahisi lakini nafurahi kumuona kwa sababu Luis ana kipaji cha hali ya juu sana.

“Ninaamini huko mbele na pengine baada ya siku 15 nitakuwa namuanzisha katika kikosi cha kwanza kila mara,” amesema Robertinho.

Makala: Harakati zashindwa kumpa maisha Pimbi
Polisi wafafanua tukio Mbunge Ngorongoro kukamatwa