Mshambuliaji kutoka nchini Ureno, Luís Carlos Almeida da Cunha ‘Nani’, mwishoni mwa juma hili atafanyiwa vipimo vya afya, kufuatia mazungumzo baina yake na viongozi wa klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki kwenda vizuri.

Taarifa zilziochapishwa kwenye toviti ya klabu ya Fenerbahce, zinaeleza kwamba kuna matumaini makubwa kwa mshambukliaji huyo kucheza ligi ya nchini Uturuki msimu ujao, kufuatia kuonyesha nia ya dhati ya kubadili mazingira ya soka lake.

Uongozi wa klabu ya Fenerbahce, unaamini usajili wa Luis Nani utawasaidia katika mipango ya msimu ujao wa ligi ya nchini Uturuki kutokana na uzoefu alio nao wa kucheza soka la ushindani.
Nani, alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sporting Lisbon ya nchini Ureno msimu uliopita, akitokea Man Utd ya nchini Uingereza na kwa sasa imedhihirika hatoweza kupata nafasi kwenye kikosi cha meneja wa Louis Van Gaal.

Hata hivyo mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alikua na matumaini makubwa ya kurejea nchini England kuitumikia klabu ya Man Utd, baada ya kueleza dhamira hiyo mieizi iliyopita.
Akiwa nchini kwao Ureno msimu uliopita, Luis Nani aliifungia Sporting Lisbon mabao 12 katika michezo 35 aliyocheza.

Mbatia atoa Msimamo Wake Kuhusu UKAWA
Pinda Awashukia ‘Wazee Wa Fitina’ Mchakato Wa Uchaguzi