Mshambuliaji kutoka nchini Uruguay, Luis Alberto Suárez Díaz amesema hatatizwi na kauli inayodai hakuwa chaguo la kwanza la FC Barcelona wakati akisajiliwa mwaka 2014 akitokea Liverpool.

Suarez, amesema kauli hiyo haina msingi kwake na anaamini huenda inazungumzwa kutokana na baadhi ya vyombo vya habari kusaka namna ya kuripori story zao.

Amesema hata kama jambo hilo ni kweli, bado anachofahamu yeye ana umuhimu mkubwa katika klabu ya Barcelona kwa sasa, kutokana na mambo mazuri anayoendelea kuyafanya.

“Sijali kama sikua chaguo lao, achana na habari hiyo. Tuseme sasa nataka kuhama, utasikia habari hiyo kwamba ninatakiwa kuwa wa kwanza kuuzwa? Najua hakuna anayetamani niondoke leo na hiyo ndio tofauti na maneno na vitendo,” amesema Suarez.

Aliyewahi kuwa mkurugenzi wa michezo wa zamani wa Barcelona, Andon Zubizarreta alisema klabu yake, iliamua kumsajili Luis Suarez kwa sababu mchezaji ambaye alikuwa chaguo lao la kwanza hakuwekwa sokoni.

“Ikasemwa kwamba kauli hii imewashangaza wengi ila ndio ukweli, Luiz Suarez hakuwa chaguo la kwanza katika usajili wa Barcelona.” Alisema Zubizarreta

Zubizarreta ameongeza kwamba waliekua wanamuhitaji kwa kipindi hicho ni mshambuliaji kutoka nchini Argentina na Man City, Sergio Aguero, lakini walikukabiliwa na kisiki cha kumng’oa Etihad Stadium.

Sergio Aguero

“Tulikuwa na machaguo machache, chaguo letu la kwanza halikuwa Suarez, yeye mwenyewe anajua hili.”  “Tulijaribu kumsaini Aguero lakini ikashindikana na mpaka kufikia hapo hatukuwa na uamuzi mwingine wa kufanya zaidi ya kumsajili Suarez.”

Zubizarreta pia anasema, suala la Suarez kufungiwa kwa kumng’ata beki wa Italia, Giorgio Chiellini liliwapa nafasi zaidi wao kwa sababu timu nyingine ziliamua kuachana na mipango yao ya kumtaka mchezaji huyo. Aliongeza:

“Wakati tupo kwenye majadiliano ya Liverpool likatokea lile sakata la Suarez na Chiellini.” “Suala hili lilileta mashaka makubwa kwenye vichwa vya viongozi wa timu nyingine waliokuwa wakimtaka Suarez.”

“Tabia yake ilikuwa kwenye mjadala mkubwa na hakuna aliyekuwa anajua atafungiwa kwa muda gani, muda huohuo ndipo nafasi ya kumsajili ikawa kubwa na tukakamilisha kila kitu.”

Gundogan Kumfuata Jurgen Klopp Liverpool
Alex Sandro Lobo Silva Ajipigia Debe Kwenda Man City