Kocha wa Inter Miami CF, Gerardo “Tata” Martino amethibitisha klabu yake kuendelea kutaka kumsajili mshambuliaji mkongwe, Luis Suárezi.

Akizungumza na vyombo vya habari Martino alisema wanaendelea kutathmini uwezekano wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Uruguay.

“Katika uchambuzi wetu wa msimu Ujao, na mahitaji ambayo tunaweza kuwa nayo, tuna uchambuzi na tunamhitaji Suarez,” alisema Martino.

“Wakati ukifika wa kufanya hali ya Suárez kuhusiana na Inter Miami rasmi, tutakuwa tayari kwenda katika mwelekeo unaolingana.”

Kama ilivyothibitishwa mapema mwezi huu na kocha wake wa sasa wa Grêmio, Renato Gaucho, Suárez ataondoka katika klabu hiyo yenye maskani yake Porto Alegre mwishoni mwa msimu wa Serie A ya Brazil Desemba, licha ya kuwa katika nusu tu ya mkataba wake wa miaka miwili.

“Alikuwa mtu aliyepitia hapa na sio tu alijidhihirisha huko Grêmio, lakini ninaamini Brazil yote inaitambua,” alisema Gaucho.

“Nimekuwa na furaha kufanya kazi naye. Tutamkumbuka sana.”

Suárez mfungaji bora wa muda wote wa Uruguay akiwa na mabao 68 katika mechi 137 alizocheza na La Celeste, kwa sasa ndiye mfungaji bora wa Grêmio msimu huu akiwa na mabao tisa katika michezo 27 ya ligi.

FEMATA wakutana kuzikataa chokochoko
Sancho anakaribia kuondoka Man Utd