Kiungo kutoka nchini Croatia na mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid Luka Modric, ametangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka barani humo (UEFA Player of the Year).

Modric ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo katika hafla ya upangaji wa makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2018/19, iliyofanyika mjini Monaco nchini Ufaransa leo jioni

Kiungo huyo ambaye alikua chachu ya klabu ya Real Madrid kutwaa ubingwa wa tatu mfululizo wa barani Ulaya msimu wa 2017/18, ametwaa tuzo hiyo na kuwashinda wapinzani wake Cristiano Ronaldo wa Juventus FC na Mo Salah wa Liverpool.

Tuzo hiyo inakua ya pili kwa kiungo huyo, baada ya kutajwa kama mchezaji bora wa fainali za kombe la dunia zilizochezwa nchini Urusi kuanzia Juni 14 hadi Julai 15 mwaka huu.

Mbali na kutajwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka, kiungo huyo mwenye urmi wa miaka 32, pia ametwaa tuzo ya kiungo bora wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu wa 2017/18.

Tuzo ya kipa bora imekwenda kwa mlinda mlango wa Real Madrid Keylor Navas

Beki bora: Sergio Ramos (Real Madrid)

Mshambuliaji bora: Cristiano Ronaldo (Real Madrid/Juventus FC)

Didier Deschamps atangaza kikosi cha maangamizi
Makundi ligi ya mabingwa Ulaya hadharani