Timu ya taifa ya Ubelgiji imefuzu kucheza fainali za kombe la dunia 2018 zitakazounguruma nchini Urusi, kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja waliouchuma dhidi ya Ugiriki usiku wa kuamkia leo.
Bao la ushindi lililofungwa na mshambuliaji wa klabu ya Man Utd Romelu Lukaku katika dakika ya 74, liliivusha nchi hiyo ya barani Ulaya hadi kwenye fainali hizo, ambazo zinasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka duniani kote.
Jan Vertonghen aliifungia Ubelgiji bao la kwanza dakika ya 70, lakini dakika tatu baadae Zeca leveling aliisawazishia Ugiriki.
Ushindi huo unaiweke Ubelgiji kileleni mwa kundi H kwa kufikisha point 22 wakifuatiwa na Bosnia-Herzegovina wenye point 14.
Tofauti ya point nane iliopo baina ya timu hizo, inatoa nafasi kwa Ubelgiji kufuzu moja kwa moja kwenye fainali za kombe la dunia, kwani haiwezezi kufikiwa na timu yoyote iliyopangwa kwenye kundi H.
Timu nyingine zilizopo kwenye kundi H ni Cyprus, Estonia na Gibraltar.
Ubelgiji wanajiunga na mataifa mengine yaliyofanikiwa kufuzu mpaka sasa ambayo ni, Brazil, Mexico, Iran, Japan pamoja na wenyeji wa fainali za kombe la dunia Urusi.
Matokeo ya michezo mingine ya kuwania kufuzu ukanda wa barani Ulaya
Kwa mantiki hiyo Ubelgiji inakua nchi ya kwanza kutoka barani Ulaya kutinga fainali za kombe la dunia, kupitia michezo ya kuwania kufuzu.