Mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji na Klabu ya Inter Milan Romelu Lukaku, amefunguka kuwa akili yake ipo kuangalia namna gani anaisaidia klabu hiyo wa mjini Milan, na ndipo ataanza kufikiria hatma yake.

Lukaku anaitumikia Inter Milan kwa mkataba wa mwaka mmoja, akitokewa Chelsea, ambayo huenda ikamrudishamwishoni mwa msimu huu.

Lukaku amesema malengo yake kwa sasa ni kuona timu yake hiyo inapata mafanikio ndipo atakuja kuangalia kuelekeo wake wa msimu ujao.

“Kuhusu hatma yangu? Kwanza natakiwa kuwa makini kwa kile nitakachokisema, ila kwa sasa nataka kuangalia nini nafanya nikiwa na Inter kwa kuonesha ubora kwa kila mechi ambayo ipo mbele yangu kuhakikisha tunapata ushindi kwanza.”

“Mimi nimekuwa nikipambana kuwa katika ubora wangu na hapa Inter nimekuwa na uhusiano mzuri na mashabiki kitu ambacho ni kizuri na kuhusu wapi naelekea itafahamika wakati ukifika,” amesema Lukaku

Chelsea walimsajili Mshambuliaji huyo kwa Pauni Milioni 90.5, lakini alishindwa kuonesha cheche zake kikosini hapo kiasi cha kutolewa kwa mkopo na haifahamiki kama atarejea Chelsea atauzwa ama la.

Wanotesa watu wachukuliwe hatua- Majaliwa
Chalamila athibitisha ongezeko la mmoja kifo cha Maburg