Hofu imetanda katika kambi ya maandalizi ya klabu ya Everton baada ya mshambuliaji wa klabu hiyo Romelu menama Lukaku, kuumia katika mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Dundee Utd uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo.

Lukaku alishindwa kumaliza mchezo huo, baada ya kupata maumivu ya nyama za paja, hali ambayo ilimsababisha kutoka uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji mwingine.

Taarifa kutoka Goodson Park, zinasema kwamba mshambuliaji huyo hii leo atafanyiwa vipimo ili kujua ameumia kiasi gani, na kama atakuwa na matarajio hafifu ya kurejea mapema kuna hati hati akaukosa mwanzo wa msimu wa ligi ya nchini England ambayo itaanza kutimua vumbi lake mwishoni mwa juma lijalo.

Meneja wa Everton Roberto Martinez amesema hana budi kufanya subra ya kujua matokeo ya vipimo vywa mshambuliaji huyo, ambayo yatapatikana muda mchache kuanzia sasa na ndipo atakuwa na lolote la kuzungumza kuelekea mwanzoni mwa msimu.

Tayari meneja huyo kutoka nchini Hispania ameshawapoteza Gerard Deulofeu pamoja na Steven Pienaar baada ya kupatwa na maumivu wa nyama za paja katika michezo iliyopita ya kujipima nguvu, na tayari imedhihirika wawili hao hawatokau sehemu ya kikosi cha Everton mwanzoni mwa msimu.
Katika mchezo uliocheza usiku wa kuamkia hii leo, Everton waliibuka na ushindi wa mabao mawili kwa sifuri yaliyofungwa na Ross Barkley pamoja na Conor McAleny.

Protektion von Informationen gegenwärtig
Lowassa kuchukua Fomu ya Kugombea Urais Kesho