Klabu ya Chelsea imefuta uchunguzi kutoka kwa Juventus kuhusu mkataba wa mkopo wa mshambuliaji kutoka nchini Ubelgiji Romelu Lukaku.

Lukaku amerejea hivi punde kutoka kwenye mkataba wa mkopo na Inter na anatarajiwa kuondoka Chelsea majuma machache yajayo baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Mauricio Pochettino kwa ajili ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya nchini Marekani.

Inter walikuwa wakiongoza mbio za kuinasa saini yake, lakini kwa mshtuko waliachana na harakati za muda mrefu za kumnasa mshambuliaji huyo, huku kukiwa na tuhuma kwamba amekuwa akifanya mazungumzo na Juventus, licha ya Lukaku kudai kwa faragha na hadharani kwamba hatawahi kuhamia timu nyingine ya Italia.

Mchezaji mwenzake wa zamani wa Inter Lautaro Martinez hivi karibuni alikiri kuwa amesikitishwa na tabia ya Lukaku msimu huu wa majira ya joto.

Mikutano ya Lissu: mambo bado magumu
Pochettino ataka kiungo mzoefu