Katika kuhakikisha kuwa Serikali inawatumikia na kuwatendea haki wananchi katika kutoa huduma mbalimbali za kijamii, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemsimamisha kazi  Afisa Mipango Miji Mkoani Lindi baada ya kunyang’anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.

Lukuvi amefikia hatua hiyo mara baada ya kuonekana kuwa utaratibu wa umilikishwaji ardhi haukufuatwa, hivyo kuonekana kwa mianya ya rushwa.

“Kama nyie mmeshindwa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa Serikali, naagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali,”amesema Lukuvi

Aidha, Lukuvi amelishauri Shirika la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo ina changamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla.

DC Kapufi awafunda waandishi wa habari Geita mjini
Vifo Vyaongezeka Maandamano Kupinga Maamuzi ya Serikali Venezuela