Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amekanusha kauli za baadhi  ya viongozi wa vyama vya siasa kuwa kuna baadhi ya viongozi wamepora ardhi ikiwemo ardhi ya eneo la Mbarari mkoani Mbeya na kusisitiza kuwa kati ya viongozi waliotuhumiwa hakuna hata kiongozi mmoja  aliyepora ardhi.

Lukuvi amesema umilikishaji ardhi nchini unafuata sheria na serikali haina ubaguzi katika kumilikisha mtu yeyoye ardhi huku akiweka wazi kuwa  umilikishaji ardhi kwa mtu yeyote hauna kikomo.

“Serikali ya awamu ya tano haina ubaguzi wa kumilikisha ardhi na mwananchi yeyote bila kujali itikadi ya chama cha siasa anaweza umilikishwa,” amesema Lukuvi.

Amesema Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kushughulikia masuala ya ardhi ikiwemo lile la kuvibakisha vijiji 920 kati ya  975 vilivyokuwa kwenye hifadhi na kuwa serikali inaangalia namna ya kuvibakisha vijiji vingine 55 vilivyosalia.

Waziri Lukuvi amewaasa wananchi wote waliomilikishwa ardhi kuhakikisha wanafuata sheria na kusisitiza kuwa, sheria za ardhi zimewekwa ili kutekelezwa na wasiozifuta watafutiwa umiliki na kupatiwa watu wengine.

Makubaliano ya kimyakimya ACT-Wazalendo na CHADEMA
Waziri mkuu ashindwa kuunda serikali - Lebanon