Katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki yao ya kumiliki Ardhi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewaonya maafisa ardhi na mipango miji wasio waadilifu wanaosababisha kero za migogoro ya ardhi nchini kuacha mara moja tabia hiyo vinginevyo watashughulikiwa.

Ameyasema hayo mapema hii leo mkoani Iringa wakati wa Uzinduzi wa Master  Plan ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambayo inatarajiwa kuwa mkobozi wa kutatua migogoro ya Ardhi.

Amesema kuwa mchezo huo wa ufisadi ambao umekuwa ukitumiwa miaka yote na maofisa ardhi nchini ameubaini na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutokubaliana na ramani za maeneo mapya zinazoletwa na wataalam hao bila ya wao kufika maeneo husika na kuonyeshwa maeneo hayo ili kujiridhisha.

Aidha, amesema kuwa ufisadi unaofanywa na maafisa ardhi nchini kwa kupima viwanja hewa kwa ajili ya maslahi yao na kusema kuwa mbinu ambayo wamekuwa wakiitumia  kuiibia  serikali amekwisha  ibaini na hata kubali kuona mbinu hiyo inapewa nafasi katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli .

“Unakuta kwenye ramani inayonyesha kuna bonde kubwa lisilofaa kujengwa kumbe ukifuatilia eneo hilo ni zuri kuliko yote na hapo wametenga viwanja vya kuuza, Unakuta  ukipima kuna viwanja vingi na vizuri ambavyo ni vyao wao wanachofanya baada ya kuuza viwanja halali za Halmashauri hurudi kupima maeneo hayo walioonyesha ni mabonde na kugawana wao kwa ajili ya kuuza kwa faida yao,”amesema Lukuvi

 

Hata hivyo ameongeza kuwa ujenzi holela katika miji na halmashauri imesababishwa na ukilitimba wa utoaji wa vibali kwa wakati na ndio sababu ya wananchi kuvamia maeneo yasiyo pimwa japo kuanzia sasa  wote  waliopo katika maeneo yasiyo pimwa  watapewa leseni ya makazi ya miaka mitano na watalipa kodi ya ardhi na baada ya miaka mitano wahakikishe  wamepimiwa  ili  kupewa hati.

 

Video: Makamba ateta na wadau wa mazingira Dar
Serikali yapanga mikakati mizito kukabiliana na tatizo maji