Muigizaji Elizabeth Michael aka Lulu amepanga kuachia filamu yake mpya aliyoibatiza jina ‘Ni Noma’, aliyoiandaa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tangu alipota filamu yake ya mwisho.

Lulu ameiambia Ayo TV kuwa amemshirikisha muigizaji wa kiume, Dude pamoja na wasanii wengine wapya ambao hawajapata majina makubwa kwenye tasnia.

“Ni movie yangu mpya, actually ndiyo itakuwa movie yangu mpya tokea movie ya mwisho ambayo nimeitoa mwaka jana mwezi wa 3, kwa hiyo kimekuwa ni kipindi cha mwaka mzima sijafanya movie,” alifunguka.

Size 8 Amuandikia Mumewe Ujumbe Mtamu Baada Ya Kupewa Zawadi
Keko Wa Uganda Atimuliwa Coke Studio Baada Ya Kuvuruga