Beki wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda amesema kila nafasi anayoipata ya kucheza kwake ina tafsiri ndoto za muda mrefu alizonazo zikiishia kwa vitendo, akitamani kucheza kwa kiwango kikubwa ndani na nje.
Nyota huyo aliyewahi kukipiga KMC FC, amesema jinsi ambavyo kikosi cha Azam FC kilivyo na mastaa wenye ushindani mkali, ambao kila wakati unamfanya ajitume na kuona hana wakati wa kubweteka.
“Kwanza ushindani wa namba unanifunza kila wakati, ninapoaminiwa kucheza maana yake kocha ameona kitu kwangu, hivyo inanilazimu kujituma ili kufanya kile kinachotazamwa kwangu,” amesema Lusajo.
Amesema tangu aanze kucheza soka kwa kujitambua, alitamani awe mfano kwa wengine ambao wanatajwa kama kigezo bora kwa vijana, kulingana na rekodi walizoziandika kwenye soka.
Wakati nacheza kikosi B ndoto yangu ilikuwa kucheza kwa kiwango ambacho wengine wanaokuja nyuma yangu watamani ninachofanya kwani na mimi nilikuwa napenda walivyokuwa wanacheza kina Kelvin Yondani na wengine, Juma Nyoso na kaka zangu wengine wengi,” amesema na kuongeza;
“Kutokana na kucheza nafasi tofauti, wakati mwingine nacheza namba mbili na kati,” amesema.