Moja kati ya Wilaya kumi na moja za Mkoa wa Tanga nchini Tanzania, Wilaya hii imepakana na Kenya kwa upande wa kaskazini-mashariki na kwa upande wa mashariki imepakana na Wilaya ya Muheza, upande wa kaskazini-magharibi imepakana na Mkoa wa Kilimanjaro.
Pia Wilaya hii, upande wa magharibi imepakana na Wilaya ya Korogwe na kusini imepaka na Wilaya ya Bumbuli ukiwa ni Mji Mkuu wa Wilaya na mkubwa Mkoani Tanga, panaitwa Lushoto usiache kutembelea Mkoa wa Tanga.
Lakini licha ya uzuri na umaarufu wa mji huo, bado zipo changamoto kadhaa zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo ikiwemo matukio ya ajali huku wenyeji wakisema Jeshi la Polisi linaendelea kuwawajibisha madereva kutokana na kile wanachokiita uzembe na kutokuzingatia sheria za usalama barabarani.
Wanasema licha ya suala hilo, pia Serikali inatakiwa kujitathmini kwa kuzipitia upya sheria za usalama barabani huku ikiitazama na miundombinu ya barabara ambayo nayo si rafiki kwa madereva kwani ajali za mara kwa mara hutokea.
Wakati wa ukoloni wa Wajerumani (1890 hadi 1918), eneo hilo lilikuwa maarufu kwa walowezi, kwa hivyo Mashamba makubwa na mashamba yaliundwa, na wilaya ilithaminiwa kwa hali ya hewa yake ya kupendeza ikipambwa na milima ya yenye miti mirefu na mandhari ya kuvutia.
Zipo baadhi ya changamoto ambazo huwa zinawakabili watu kwenye jamii na inafika wakati wanakata tamaa kabisa ya maisha, lakini kwa binadamu wa kawaida hana budi kupambana na changamoto hizo ili kuhakikisha anafikia malengo yake aliyoyakusudia.
Hakuna kitu kibaya kama kukata tamaa, na siku zote elewa kwamba changamoto ni sehemu ya maisha na pia jaribu kufuatilia mambo yanayokufurahisha, jambo ambalo Wanalushoto limewafanya wasikate tamaa, wanapambana na wanasisitiza kwamba watafikia malengo waliyoyakusudia.