Uongozi wa klabu ya Zesco United FC ya nchini Zambia, umeachana na kocha George Lwandamina, baada ya kuafikiana kuvunjwa kwa mkataba wa pande hizo mbili.
Uamuzi huo umekuja baada ya msimu mbovu kwa Zesco Utd wakiukosa Ubingwa na kuikosa nafasi ya kushiriki Michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika msimu mpya wa 2020/21. Mabingwa wakiwa ni mahasimu wao Nkana FC huku Zesco Utd wakimaliza nafasi ya tano msimu uliopita wakishinda michezo 13, wakitoka sare mara 8 na kufungwa michezo 6.
Mtendaji mkuu wa Zesco Utd FC Richard Mulenga amemshukuru Lwandamina kwa kazi yake iliyotukuka klabuni hapo, na amemtakia kila la kheria katika masha yake baada ya kuondoka. Kocha huyo aliitumikia klabu hiyo kwa vipindi viwili tofauti.
Lwandamina ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Young Africans kuanzia mwaka 2016-2018 na baadae alichana na klabu hiyo na kurejebia.
Kabla ya kutua nchini Lwandamina alikua kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zambia mwaka 2015-2016., ambapo aliteuliwa kuifanya kazi hiyo akitokea Zesco Utd kuanzia mwaka 2014-2015.
Katika miaka mitatu aliyokaa George Lwandamina tokea alipoachana na klabu ya Young Africans, aliiwezeaha Zesco kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu ya Zambia na taji moja la ABSA.
Wakati huo huo aliyekua mshambuliaji wa Young Africans David Ndama Molinga amesajiliwa na klabu ya ZESCO United akiwa mchezaji huru, baada ya kuachwa na mabingwa hao wa kihistoria katika soka la Bongo mwanzoni mwa mwezi Agosti.
Falcao aliondoka Young Africans hukua kiacha heshima ya kuwa mfungaji bora wa klabu hiyo kw amsimu wa 2019/20, ambao ulimalizia kwa Simba SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu mfululizo.