Kiungo mpya wa mabingwa wa Soka Tanzania Bara Taddeo Lwanga amejumuishwa kwenye kikosi kilichosafiriki kuelekea Zimbabwe, kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya mabingwa Barani Afrika dhidi ya FC Platnum.

Lwanga alisajiliwa Simba SC majuma mawili yaliyopita, mara mbili alionekana jukwaani wakati timu yake ilipocheza michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Polisi Tanzania na KMC FC, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Taarifa zinaeleza kuwa Lwanga amesafiki na timu, huku akichukua nafasi ya kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ghana  Bernard Morrison alieachwa jijini Dar es salaam.

Endapo kiungo huyo kutoka nchini Uganda, atacheza mchezo dhidi ya FC Platnum utakua mchezo wake wa kwanza kuitumikia Simba SC, tangu aliposajiliwa klabuni hapo, akichukua nafasi ya Mbrazil Gerison Fraga Vieira alieachwa kwa sababu ya kuwa na majeraha ya muda mrefu.

Hata hivyo Lwanga huenda akatumiwa na Simba kwenye michuano ya kimataifa pekee, kufuatia kanuni za usajili wa Tanzania kuibana klabuni hiyo, kwa kuitaka kila klabu kuwa na wachezaji 10 wa kimataifa, idadi ambayo imetimia kwa wekundu hao.

Mbali na Morrison nyota mwingine ambaye ameachwa ni Charles Ilanfya ambaye sio chaguo la kocha Sven licha ya uongozi kuweka wazi kwamba usajili wa mchezaji huyo kutoka Klabu ya KMC FC ilikuwa ni pendekezo la kocha huyo kutoka nchini Ubelgiji.

Wawili kuongezwa Young Africans
Polisi walivyozima sherehe ya ufuska Dar