Hatimaye uongozi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Simba SC umemtambulisha kiungo kutoka nchini Uganda Taddeo Lwanga.

Kiungo huyo mkabaji ametambulishwa na klabu hiyo kupitia kurasa zake za mitando ya kijamii, ambapo picha zilizoanikwa hadharani zilimuonesha akiwa na makamu mwenyekiti wa Simba SC Mwina Mohamed Seif Kaduguda (Simba Wa Yuda).

Taarifa zilizochapishwa kwenye kurasa za mitandao ya Simba SC zimeeleza kuwa, Lwanga amesaini dili la miaka miwili, na atavaa jezi namba nne, iliyokua ikitumiwa na kiungo kutoka Brazil Gerison Fraga.

Kiungo huyo amewahi kuzichezea timu za Express FC, SCV Kampala, Vipers FC na Tanta FC hivyo uzoefu wake na uwezo wake ndani ya uwanja ni sababu ya kupewa dili ndani ya Simba.

Lwanga alikuwa akiwindwa na Simba SC kwa muda mrefu baada ya kiungo Gerson Fraga kupata majeraha ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Fraga aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United na nafasi yake ilichukuliwa na Said Ndemla ambaye ni mzawa.

Usajili wa Lwanga unatokana na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kutoa nafasi za wawakilishi wa mashindano ya kimataifa kusajili wachezaji 10 ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo.

Azam FC yawatumia salamu Gwambina FC
Msola: Mchakato wa mabadiliko umepiga hatua kubwa