Viongozi wa kundi la waasi la M23, wamekutana na msuluhishi wa kanda Rais wa zamani wa Kenya, Uhuru Kenyatta mjini Mombasa na kukubali kuondoa wapiganaji wao kutoka jimbo la Kivu Kaskazini lililopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.

Mkutano huo, umefanyika baada ya wanaharakati wa eneo la mashariki mwa DRC kulitaka jeshi la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF), kuchukua hatua za kijeshi dhidi ya waasi wowote wanaolipinga jeshi la Kongo, kitu ambacho kinaweza kuongeza mivutano zaidi.

Mjumbe wa amani wa jumuiya ya Afrika mashariki kuhusu amani katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, rais mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta baada ya mkutano na viongozi wa ngazi ya juu wa kundi la waasi la M23. Picha ya VOA.

Hatua hii, inakuja ikiwa ni wiki kadhaa baada ya waasi wa M23 kuomba kuelezea matatizo yao kwa Kenyatta, ambaye ni mpatanishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huku pia mkutano wa kimataifa kwa eneo la Maziwa Makuu (ICGLR) ukijaribu kuleta usuluhishi mashariki mwa DRC.

Mwenyekiti wa kundi la M23, Bertrand Bisimwa  amesema wao walitengwa katika vikao vya mazungumzo na serikali ya Kongo mpaka watakapo jiondoa katika maeneo yote wanayoyashikilia na sasa wametangaza nia ya kutaka amani na kushirikiana na Jeshi la Afrika Mashariki.

Nikilala kitandani asubuhi najikuta makaburini: Mwl. Nondo
Kagame awatumia ‘Kombora’ wanaotaka kumpindua