Serikali imepanga kuanza kuwatoza kodi washereheshaji wa harusi (Ma-MC), wapishi katika sherehe mbalimbali na wamiliki wa kumbi za harusi ili kuongeza pato la taifa.

Mpango huo wa Serikali uwekwa wazi hivi karibuni na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), Richard Kayombo alipozungumza na waandishi wa habari.

Kayombo alieleza kuwa serikali inafahamu kuwa washereheshaji hao na watu wanaofanya biashara ya kukodisha kumbi za harusi wanapata kiwango kikubwa cha fedha lakini hawalipi kodi. Hivyo, umeandaliwa utaratibu wa ulipaji kodi ambao utasaidia kuwabaini walipe kodi na kuchagia pato la taifa ikiwa ni jitihada za kuondokana na utegemezi.

Ukumbi

“Tunajua wapo ma-mc, wapishi wakubwa na hata watu wanakodisha kumbi wanaingiza kiwango kikubwa cha fedha, lakini hawalipi kodi, ni wakati mwafaka nao kuanza kulipa kodi,” alisema Kayombo

Aliongeza kuwa kama wafanyabiashara wengine, wanapaswa kuwa na namba ya utambulisho wa biashara (TIN Namba) ambayo itawasaidia kutambulika katika mfumo wa Mamlaka hiyo.

“Tunawaomba watupe ushirikiano, hivi sasa unaandaliwa utaratibu mzuri wa kukutana nao kupitia chama chao ili kuwaeleza utaratibu huu mpya ambao utasaidia kujenga nchi yetu na kuwa na maendeleo zaidi,” alieleza.

Pep Guardiola Meneja Mpya Etihad Stadium
Kikwete apata uteuzi mwingine mzito wa kimataifa