Hospitali ya Taifa ya imepitishwa kupokea, na kupewa kushughulikia kiafya zinazoweza kujitokeza kwa wachezaji watika wa Fainali za Mataifa ya Barani Afrika ‘AFCON 2027’, ikiwa Afrika Mashariki itapewa ridhaa ya kuwa mwenyeji wa Fainali hizo.
Muhimbili nafasi ya dharura za Hayo yalisemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Saidi Yakub, aliyeambatana na jopo la wakaguzi kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’.
Wakaguzi hao wapo nchini kwa lengo la kukagua miundombinu muhimu vikiwemo viwanja vya michezo, hoteli, viwanja vya ndege na hospitali.
Wakaguzi hao jana katika ukaguzi wao walitembelea Hospitali ya Muhimbili na kufanya ukaguzi katika idara ya magonjwa ya dharura na ajali, mashine za kisasa za uchunguzi huku wakipata maelezo mazuri kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi.
Katika ukaguzi huo, Profesa Janabi aliwaeleza wakaguzi kuwa, MNH ina uwezo, utayari wa kupokea na kutatua dharura zozote zinazoweza kujitokeza.
Alisema ukaguzi umekamilika kwa Muhimbili na imekidhi vigezo vilivyotakiwa, zinasubiwa ambazo wakaguzi wameziomba kwa lengo la kukamilisha ukaguzi wao.
Amesema kijiografia katika eneo ilipo Muhimbili, kuna hospitali mbili za ubingwa wa juu ambazo ni Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI), ambazo kwa pamoja zina uwezo wa kutatua changamoto yoyote inayoweza kujitokeza.
Tanzania kwa kushirikiana na Kenya na Uganda, zimeomba kuandaa fainali hizo huku zikishindana na Algeria, Botswana na Misri.