Waziri wa Madini, Doto Biteko, amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa yote ya kimadini nchini kuimarisha mahusiano baina yao na viongozi wengine wa Serikali waliopo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya, watendaji wa kata na viongozi wa vijiji wanakohudumia.
 
Amesema kuwa wao ndio sura ya Wizara katika mikoa na Wilaya wanazozisimamia  na kuwataka kuweka historia nzuri kwenye maeneo yao. “Likitokea jambo baya lolote sote tunachafuka hivyo tuwe makini katika kujenga taswira njema ya sekta yetu” Biteko amesisitiza.
 
Amesema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 ambao upo katika almanac ya Tume ya Madini ya Mwaka 2021/2022 wenye lengo la kujadili juu ya uboreshaji wa mikakati mbalimbali ya namna ya kufikia na hata kulivuka lengo la kukusanya Shilingi 650,000,000,000 walilopangiwa na Serikali kwa mwaka huu wa fedha.

“Suala hili ni jema, na Wizara ya Madini inawaunga mkono na kama ilivyo ada itaendelea kuunga mkono juhudi hizi ambazo zina tija kwa Sekta ya Madini katika kuhakikisha Sekta inafikia mchango wa asilimia 10 kwenye Pato la Taifa ifikapo 2025” ameongeza Biteko.

Amesema kiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni kuifanya Sekta ya Madini inaendelea kuwa kinara kwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kubainisha kikao hicho ni muhimu kwani kimewahusisha wataalamu wanaosimamia kwa ukaribu zoezi la ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.
 
Aidha, Waziri Biteko amewataka watendaji hao kutumia mkutano huo kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kutokana na mazingira tofauti tofauti waliyotoka, pia kuchangia kwa uhuru na uwazi ili kutoa nafasi kwa viongozi kuona namna bora ya kushirikiana nao katika kutatua changamoto watakazoziibua.

“Wizara imepewa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 650,000,000,000 ni  kubwa lakini msivunjike moyo kaendeleeni kufanya kazi ili kuifanya Sekta ya Madini iendelee kuwa kinara katika kuchagiza ukuaji wa uchumi wa nchi,” Amesema Waziri Biteko.

Pamoja na hayo Waziri Biteko, amewapongeza  Maafisa hao kwa namna wanavyofanya kazi katika maeneo yao na kueleza kunapokuwa.

Wizara ya ujenzi na JWTZ kukuza uhusiano
Masau Bwire awakumbusha Young Africans