Rais mteule wa Marekani Joe Biden ametangaza timu ya maafisa wanawake waandamizi mawasiliano ya Ikulu ya nchi hiyo katika kile amabcho ofisi hiyo imekieleza kuwa ni historia ya nchi.

Biden na makamu wa rais mteule, Kamala Harris wamefanya uteuzi wa aina hiyo kutaka kusisitiza wanajali utofauti katika jamii kabla ya kula kiapo Januari 20.

“Maofisa hawa wa masiliano walio na sifa na waandamizi wanaweka dhana ya utofauti katika kazi zao na wenye nia moja ya kulijenga tena taifa hili.”amesema Biden

“Ninajivuna kutangaza leo timu ya kwanza ya nmaofisa waandamizi iliyojaa wanawake,” amesema Biden 

Miongoni mwa walioteuliwa ni Jen Psaki (41), ambaye atachukua jukumu la katibu wa mawasiliano wa ikulu, ameshikilia nafasi kadhaa za juu, ikiwemo ya mkurugenzi wa mawasiliano w aikulu wakati wa utawala wa Barack Obama na Biden.

Bedingfield pia alikuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Biden wakati akiwa makamu wa rais.

Wengine walioteuliwa ni pamoja na Ashley Etienne anayekuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Harris na Symone Sanders anayekuwa mshauri mwandamizi na msemaji mkuu wa Harris.

Tobar ametangazwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa ikulu na Karine Jean Pierre anakuwa naibu katibu wa habari naye Elizabeth Alexander ametangazwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa mke wa rais, Lady Jill Biden.

Somalia yamrudisha nyumbani balozi wake na kumfukuza wa Kenya
Azam FC kujiuliza kwa Biashara United Mara