Maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa wamewasili nchini Afghanistan kufanya mazungumzo na utawala wa Taliban juu ya ubaguzi wa kijinsia na kushinikiza haki za wasichana na wanawake wa Taifa hilo.
Msemaji wa umoja huo, Farhan Haq amesema ujumbe huo umeongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed na Katibu Mkurugenzi wa masuala ya Wanawake kwenye Umoja wa Mataifa, Sima Bahous.
Amesema, ziara yao imejiri ikiwa ni siku chache baada ya mbunge wa zamani kuuawa nyumbani kwake mjini Kabul na tangu utawala wa Taliban ulipochukua madaraka miezi 17 iliyopita, kundi hilo limewawekea wasichana na wanawake masharti magumu.
Masharti hayo ni pamoja na kuuwapiga marufuku kusoma katika shule za sekondari na vyuo vikuu na kuwazuia kutembelea mbuga na bustani za umma huku ikiwapiga marufuku mashirika ya misaada kuwaajiri kazi wanawake.