Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt Phillip Mpango amewaagiza wachimbaji wa madini kuzingatia kanuni za mazingira ili kuepuka uharibifu wa kimazingira unaoweza kuletwa na kazi hiyo.

Dkt Mpango amesema hayo jana wakati akihutubia katika mkutano wa kimataifa wa uwekezaji katika sekta ya madini uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Akitaja Maagizo hayo Dkt. Mpango amewataka Wawekezaji katika miradi ya ubia na Serikali waharakishe utekelezaji wa makubaliano ili watanzania waweze kunufaika na fursa zitakazotokana na uwekezaji husika.

“Ni dhahiri kwamba, wachimbaji wa madini kwa kiwango chochote unaenda sambamba na uharibifu wa mazingira. Hivyo nawakumbusha wachimbaji wote wakubwa na wadogo kuzingatia Sheria za usimamizi wa mazingira,” aliongeza Dkt Mpango.

Amewataka Wawekezaji wote kuhakikisha kuwa shughuli za uchimbaji, uchenjuaji na uchakataji wa madini zinatekelezwa kwa mujibu wa Sheris na taratibu ili watanzania wanufaike na madini yao sambamba na wawekezaji kupata faida.

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na Waziri wa madini Dkt. Doto Biteko

“Wawekezaji wote na hususan wawekezaji wakubwa tunawataka wazingatie matakwa yanayotokana na tathmini ya athari kwa mazingira na jamii na kuzingatia misingi ya uzalishaji endelevu, matumizi ya mbinu bora za uzalishaji na teknolojia rafikikwa mazingira,” aliongeza Dkt. Mpango.

Akitaja akigo jingine Dkt. Mpango amesema, amewaasa wawekezaji pamoja na wachimbaji kutojihusisha na ajira za watoto na badala yake waongeze juhudi hususani katika kuhamasisha , kukuza uelewa na kujenga uwezo wa jamii na wachimbaji wadogo na hususan wanawake kwa kupitia wataalamu wa teknlojia.

Aidha amezikumbusha kampuni zote zinazowekeza katika sekta ya madini zihakikishe zinatekeleza ipasavyo takwa la Kisheria la kuandaa mipango ya ufungaji migodi na kuweka hati fungani ya urekebishaji wa mazingira.

Wadau wa Madini wakiwa kwenye mkutano

“Tunawasihi benki na Taasisi za Fedha kushirikiana na Shirika letu la Madini la taifa (STAMICO) kubuni namna bora zaidi ya kuwawezesha wachimbaji wetu wadogo wakati Serikali inalifanyia kazi suala la kuanzisha benki maalum ya madini.” Dkt Mpango.

Amesema Serikali iko tayari kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi kwa kuwa sekta ya Madini ni moja ya Sekta ya kipaumbele na Rais anafuatilia mijadala na mapendekezo yanayotolewa kupitia mikutano hiyo.

Aidha Waziri wa Madini, Dkt Doti Biteko amesema hakuna jambo ambalo litaacha kufanyiwa kazi na wizara katika yote yaliyojadiliwa.

Mkutano wa mwaka huu ni mwendelezo wa mkutano ulioanza mwaka 2019 lengo ni kujadili yanayotokea, wapi sekta ya madini inakwama na wapi inasonga mbele na matokeo yanayotokea ni kipimo cha kuendelea kukutana wadau hao

“Mikutano hii inaleta mitaji ya uwekezaji, tumehuhudia wengi wamejitokeza baada mikutano, shughuli za utafiti wa Gesi ya Helium zinaendelea kufanyiwa. Mhe. Makongoro ameleta zaidi ya makundi matatu 3 kwa ajili ya shughuli za uongezaji thamani madini. Mikutano hii inasaidia kupokea maoni, michango na hivyo kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ya madini” Dkt. Biteko.

Waziri wa Madini Dkt. Biteko

Mkutano Mkuu wa kimataifa wa sekta wa Madini Tanzania mwaka huu ulikua na kauli mbiu ‘mazingira wezeshi kwa maendeleo ya sekta ya madini Tanzania.

Diamond atuhumiwa kujihusisha na biashara ya Utumwa
Young Africans yachekelea kuikwepa Pamba FC