Serikali ameagiza bili za maji, lazima ziwe zimeidhinishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na kusisitiza kuvunja bodi zinazoendelea kutoza bili kinyume na maagizo ya serikali.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, leo jijini Arusha, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu ya bodi na menejimenti za mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira nchini.
Amesema kuna baadhi ya mamlaka za maji zinatoza bili za maji kinyume na Ewura, hali inayofanya malalamiko mengi kutoka kwa wananchi na kusisitiza kuzivunja kutokana na kukaidi maagizo ya serikali.
Waziri Aweso amesema kuwa bili za maji zisiwe za kubambikia, ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.