Mwanasiasa Mkongwe na Mbunge wa zamani wa Kilwa Kusini Seleman Bungala maarufu kama Bwege, amesema chanzo cha kujiondoka Chama cha Mapinduzi – CCM, kilitokana na amri ya kila Mwananchi ikiwemo na yeye kutakiwa kulima zao la Muhogo heka moja kwa lazima, la sivyo watafungwa.
Bungala ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano maalum na Dar24 Media Nyumbani kwake jijini Dar es Salaam na kudai kuwa jambo hilo halikumpendeza na hivyo kuchukua hatua ya kurudisha kadi kwa Katibu wa CCM katika eneo lake, huku akiwataka Viongozi kutowashurutisha Wananchi na ulimaji wa zao hilo Muhogo.
Amesema, “hilo tu lilinifanya nihame chama, unalazimishaje mimi nilime mihogo halafu nisimamie tena wananchi nao walime zao hilo kwa nguvu, sikupendezwa maana wamakonde wanasema sisi ni watoa taarifa hivyo nikalazimika kutoa taarifa na baadaye nilikamatwa, ila nilipinga.”
Bungala amefafanua kuwa, kitendo cha kupinga kukamatwa kilitokana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa wakati huo, Agustino Kyatonga Mrema kutoa amri kuwa Wajumbe wa Nyumba kumi wasikamatwe kitu ambacho kilimpa ujasiri wa kuhoji ni kwanini hatua hiyo ichukuliwe dhidi yake, wakati tamko limetolewa na Serikari