Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa TRA kupeleke watumishi katika mizani ya TANROADS iliyopo Kurasini Dar es Salam ili kurahisisha ukaguzi wa ‘seal’ pale ambapo magari yamezidisha uzito na yanahitaji kukaguliwa.

“TRA kuna foleni kwenye mizani, hakuna watu, kuanzia leo peleka watumishi pale tunataka ukaguzi uwe muda wote”. Amesema Majaliwa.

Ameyasema hayo wakati alipotembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona utendaji wa bandari hiyo.

 Aidha Kassim Majaliwa amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ihakikishe mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania (TANCIS) unafanya kazi kwa ufanisi ili kupuinguza malalamiko ya wateja kuhusu mfumo huo.

Aidha amezitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania, Mamlaka ya Bandari Tanzania na Mamlaka ya Serikali Mtandao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

ACP Marwa: Wawafikishe waharifu kwetu
Watafiti ARU wabaini fursa kwenye majitaka, kinyesi