Peasi ni miongoni mwa matunda ambayo watu hawayathamini sana licha ya kuwa na faida lukuki katika mwili wa binadamu.

Peasi ambalo linamfanano na umbo kama tufaa linafaida nyingi endapo litatumika mara kwa mara.

Tunda hili limekuwa adimu kutokana na kutostawi katika maeneo mengi hivyo watu wengi hawalifahamu na hata walionapo hawalitilii maanani kama ilivyo kwa matunda mengine kama vile ndizi, embe, papai na mengine.

Tunda hili lina faida mbalimbali katika mwili wa binadamu kama vile kukausha jasho la kwapa kwa wale wenye kutokwa na jasho jingi endapo litaliwa mara kwa mara, pia husaidia kupunguza mwasho wa koo na juisi yake ni nzuri kwa kuua mba, hutibu kibofu cha mkojo na uti wa mgongo.

Vilevile tunda hili lina Vitamin A na B ambazo husaidia kuepukana na upofu, pia husaidia kuongeza hamu ya kula na kuboresha mfumo wa fahamu, wakati mwingine tunda la peasi husafisha mishipa ya moyo na kutibu mafua ya ndege na husaidia mmeng’enyo wa chakula ufanyike vizuri.

Tunda la Peasi husaidia kuongeza kinga za mwili, kuupa mwili nguvu, hupunguza shinikizo la damu, kuzuia mafuta kuganda mwilini (cholestrol), huzuia magonjwa ya saratani, kiungulia pamoja kupunguza homa.

Disko toto, Uchomaji matairi marufuku mwakampya
Tetesi: Man City yaendelea kumuwinda Messi