Parachichi ni tunda linalofahamika na kutumiwa sana Tanzania, wengi tunatumia parachichi lakini hatujui faida za mbegu iliyo katikati ya parachichi.
Utafiti unaonyesha kuwa mbegu ya parachichi inakiwango cha asilimia 65 cha amino acids na pia ina kiwango kikubwa cha fiber ukilinganisha na vyakula vingine.
Kwanza mbegu ya parachichi huweza kuimarisha kinga za mwili kutokana na kuwa na kirutubisho kiitwacho ‘antioxidants’ hii ni kutokana mbegu hiyo na kuwa na zaidi ya asilimia 70 ya kirutubisho hicho.
Inaimarisha kinga ya mwili, hivyo husaidia kuzuia magonjwa yasikupate, muhimu sana katika kuondoa mafuta yaliyozidi mwilini ( fat burning), na inachangia kupunguza uzito kwa haraka zaidi.
Mbegu ya parachichi inazuia vivimbe ( tumors) sababu inakiwango cha Flayonol. Pia mbegu ya parachichi inatoa sumu mwilini.
Saga mbegu ya parachichi kisha changanya na maji ya uvuguvugu kisha koroga vizuri na utumie mchanganyiko huo kutwa mara 2 kwa siku.