Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli, amempongeza Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kwa kukubali kuwa miongoni mwa viongozi wa serikali inayoongozwa na Rais Hussein Mwinyi na kusema kwamba maamuzi yake yaliokoa ndoa za watu.

Rais Magufuli ameitoa kauli hiyo mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo na viongozi hao wawili waliomtembelea nyumbani kwake wilayani Chato Mkoa wa Geita , akisema kwamba maamuzi ya Maalim Seif yalikuwa ya kishujaa na yenye mwongozo wa Mungu na kwamba mwanga wa maendeleo ya Zanzibar umeanza kuonekana.

“Zipo ndoa ambazo zilivunjika hasa kule Pemba, labda mwanamke aliipigia kura CCM na mwanaume akapigia ACT, na siku Maalim Seif ameingia kwenye serikali ndoa zile zikaungana, hii maana yake maamuzi yake yameunganisha wana ndoa na yana baraka kwa Mungu”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa, “Haya mambo ya vyama yasitusumbue hata wewe Maalim Seif, ukitaka kuja kuoa CCM hapa Chato ruksa nitakutafutia, tunatakiwa sisi Watanzania tutangulize maslahi ya Taifa letu na mara nyingi maadui zetu wangefurahi kutuona tunagombana.”

Raphael Daudi anaswa Ihefu FC
Simba kufunga usajili na Chikwende