Aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amewatoa wasiwasi wazanzibar kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati yake na Dk. Ali Mohamed Shein kuwa yataleta ufumbuzi kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

Akiongea jana mjini Unguja alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria sherehe ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.AW), Maalim Seif aliwaeleza wazanzibari kuwa waendelee kuwa watulivu na wasikubali kuchokozeka kwa kauli zinazotolewa na baadhi ya watu.

“Mazungumzo yanayoendelea nategemea yataleta ufumbuzi wa haki utakaozingatia matakwa ya katiba na sheria, lakini pia maamuzi ya wananchi waliyoyatoa kwenye kisanduku cha kura yataheshimiwa Insha Allah,” alisema Maalim Seif.

Alieleza kuwa mambo mengi yanaweza kusemwa katika kipindi hiki ambayo yanaweza kuzua taharuki kwa wananchi lakini aliwataka wasikubali kuchokozeka.

Hivi karibuni, Dk. Ali Mohamed Shein alisisitiza kuwa yeye ndiye rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar.

Presha ya Bomoa Bomoa Yaua zaidi ya watu 30 Dar
David Moyes Akiri Kuitamani Man Utd