Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inataka kuhakikisha hakutakuwa na ubaguzi Zanzibar na kila mwenye haki anapata haki yake.

Amesema hayo akiwa kwenye ziara Mkoa wa Kusini Pemba amabpo amesema kuwa mivutano ya kisiasa imekuwa ikiathiri ustawi wa Zanzibar .

 “Sisi sote tuna maslahi mapana na hatma ya Zanzibar, na kama maslahi yakiwa mazuri sote tutanufaika, na maslahi yakiwa mabaya basi sote tutaathirika, hivyo lazima tutambue sisi ni ndugu na Zanzibar ndiyo nyumbani kwetu,” amesema Maalim Seif

Seif ameongeza kuwa ushirikiano katika nchi haliepukiki na Zanzibar inahitaji umoja na mshikamano. Uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, unaonyesha maendeleo ya Zanzibar yataletwa na Wazanzibar wenyewe.

“Uchaguzi mkuu umeacha majeraha makubwa kwa wananchi na hii imetokea baada ya kutokuwepo ushirikiano. Mbali na yote yaliyotokea, mimi na Rais Hussein Mwinyi, tumesafiana nia na lengo letu kwa sasa ni kujenga nchi hii, kuweka umoja na mshikamano kwa maslahi yetu na vizazi vyetu,”amesema Maalim Seif

Katibu Mkuu UN akemea utaifa chanjo ya Covid 19
Young Africans yaweka mguu sawa Mapinduzi CUP