Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuiongoza vizuri Tanzania.

Ameyasema hayo wakati akitoa salamu zake za mwaka mpya kwa Watanzania, ambapo amesema kuwa rais Dkt. Magufuli ameweza kudhibiti rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.

Amesema kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya juhudi kubwa za udhibiti wa madini ili kila Mtanzania aweze kufaidi rasilimali za nchi.

“Kweli Rais Magufuli amepambana na rushwa, amepambana na mapapa na vidagaa katika rushwa na ameimarisha nidhamu ya nchi, kwani fedha nyingi zilikuwa zinatumika kuwalipa wafanyakazi hewa,”amesema¬† Maalim

Hata hivyo, ameongeza kuwa Rais Dkt. Magufuli amefanya mengi makubwa hivyo wanasiasa wasione haya kuyasifia kwa sababu za utofauti wa kiitikadi za vyama.

 

Kangi Lugola apata pigo
JPM awatakia kheri ya mwaka mpya Watanzania