Aliyekuwa mgombea urais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamad amekiri kupokea barua ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kumtaka apeleke jina la Makamu wa Kwanza wa Rais, kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Mwanasiasa huyo mkongwe, na mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, amesema kuwa chama chao bado kinatafakari suala la kuingia kwenye serikali ya Umoja wa kitaifa (SUK), na bado hakijafanya maamuzi.

Haya yanajiri baada ya hapo jana Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi kutangaza baraza la mawaziri na kusema kuwa ametimiza utashi wa kikatiba wa kukiandikia chama kilichopata kura zinazotakiwa ili kitoe jina la mtu atakayeshika nafasi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na kuacha nafasi mbili za uwaziri kwa ajili ya chama hicho.

Suala la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar sasa limebakia kwa ACT-Wazalendo.

Exclusive: Dkt. Abbas aeleza wasanii watakavyotajirika 2020-2025
Ukweli kuhusu Tanzania kufutiwa misaada na Bunge la Ulaya