Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad leo amemtembelea Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, nyumbani kwake Salasala jijini Dar es Salaam baada ya kutoka India alipokwenda kupata matibabu.

Maalim Seif aliambatana na ujumbe wa viongozi CUF ambao ni Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho, Severina Mwijage, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Magdalena Sakaya na Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa chama hicho, Julius Mtatiro.

Viongozi wa CUF wakimuombea dua Spika wa Bunge, Job Ndugai

Viongozi wa CUF wakimuombea dua Spika wa Bunge, Job Ndugai

Spika Ndugai alimueleza Maalim Seif na viongozi alioambatana nao kuwa afya yake imemarika kwa kiwango cha kuridhisha.

Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Bunda Apokea Madawati 90 Ya Chadema Yaliyokuwa Yamekataliwa Na Madiwani Wa Ccm
Polisi kuimarisha usalama mechi ya Yanga na Mo Bejaia ya Algeria