Dhana iliyojengeka miongoni mwa wananchi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) ndiye mwenye maamuzi yote katika chama hicho na kwamba yeye ndiye Chama, imetolewa majibu na mwanasiasa huyo mkongwe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Maalim Seif ameeleza kuwa dhana hiyo sio ya kweli kwa kuwa chama hicho kina uongozi wa Baraza Kuu ambalo liko juu zaidi na ndilo ambalo hukaa na kuamua mambo yake.

Maalim Seif aliyasema hayo wakati akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua uamuzi atakaouchukua endapo CCM itafanikisha kushinikiza kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar.

“Pamoja na kwamba mnasema CUF ni Seif… sio kweli. CUF ina wenyewe, sawasawa. Na dhana ni Baraza Kuu la uongozi la Taifa. Wakitangaza inabidi tuitishe na kueleza tulichoamua,” alisema Maalim Seif.

Video: Messi Abeba Tuzo ya Ballon D’Or 2015, Avunja Rekodi
Video: Beka afunika na Cover ya 'Hello' japo hajui Kabisa Kiingereza, Hutaamini