Tume ya Afya ya China imeripoti kuwa maambukizi ya Corona virus yamepungua kutoka maambukizi 1,749 kwa jana hadi maambukizi 394 kwa siku ya leo
Idadi hiyo imepungua kutokana na miongozo mipya ya kutambua Wagonjwa wa Corona ambapo kwa hivi sasa wagonjwa wanaobainika Kliniki hawatahesabiwa tena kama Wagonjwa waliothibitika
Ili Mgonjwa kuthibitika na kuhesabiwa kama Mgonjwa wa Corona kwa sasa anatakiwa kuwa amepimwa Maabara, tofauti na hivyo atatambulika kama mgonjwa mshukiwa.
Hata hivyo idadi ya vifo kwa sasa imefikia 2,126 huku vifo 10 vikiwa vimetokea nje ya ardhi Kuu ya China (Mainland China) ambapo idadi ya Waathirika wa virusi imefikia 75,600 Ulimwenguni.
Aidha watu wawili wamefariki dunia kutokana na Corona Virus nchini Iran, na hivi ni vifo vya kwanza kuripotiwa Mashariki ya Kati
Maambukizi makubwa nje ya China yapo Nchini Korea Kusini (82), Singapore (84) na Japan (68) bila kuhesabu Waathirika 624 waliothibitika katika Meli ya Diamond Princes.