Maambukizi ya viashiria vya ugonjwa wa Malaria Nchini Tanzania yamepungua kwa watoto chini ya miaka mitano kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 7.3 kwa Mwaka 2017 hii ni kuzingatia harakati zinazo fanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja na shirika la WHO kuhakikisha wanautokomeza ugonjwa huo.
 
Akizindua takwimu zilizo tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Tanzania leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa atazindua rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017.
 
“Takwimu hizi, zinaonesha kupungua kwa kiwango cha malaria kwa kiasi kikubwa, na hii ni habari njema kwetu sote na inaonesha ni jinsi gani Serikali yenu ipo tayari kutoa kipaumbele katika kuhakikisha kuwa malaria inadhibitiwa na hatimae tuweze kuitokomezwa kabisa Ili kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa,”amesema waziri Ummy
 
Amesema kuwa utafiti huo unaonyesha mikoa yenye kiwango kikubwa cha watoto wenye malaria ni, Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3), Kagera (asilimia 15.4) na Tabora (asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na Dodoma ina kiwango kidogo cha maambukizi chini ya asilimia moja.
 
Hata hivyo, kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Albina Chuwa amethibitisha matokeo ya sasa ya utafiti huo, yanayo onyesha kuwa kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano nchini Tanzania kimeshuka kwa zaidi ya nusu kutoka asilimia 14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3.

Nguruwe wapigwa marufuku Dodoma
Wenger afunguka kilichomsukuma kung'atuka Emirates Stadium