Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa wa malaria imepungua kutoka asilimia 90 ya maeneo yenye mbu  hadi kufikia  asilimia 50  ya walioambukizwa  malaria tangu 2000 hadi 2017.

Hayo yamesemwa na Dkt. Sigsbert Mkude, ambaye ni Kiongozi wa Uchunguzi na Matibabu ya Malaria nchini (NMCP) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa Kwa miaka 15 sasa viwango vya maambukizi ya malaria vimepungua kwa zaidi ya asilimia 50 hivyo imepelekea idadi ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa malaria kupungua kwa asilimia 0 ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Aidha, akitoa takwimu hizo Dkt. Mkude amesema kuwa mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Kagera na Geita  na mikoa Kusini ambayo ni Mtwara na Lindi ndiyo inayoongoza kwa maambukizi pamoja na idadi ya vifo kwa zaidi ya asilimia 50 toka mwaka 2008 hadi 2016.

 

Hata hivyo, kwa upande wake Dkt. Charles Mwalimu ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Udhibiti wa Mbu-Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria amesema Serikali imefanya mikakati ya kudhibiti maambukizi na vifo vitokanavyo na ugonjwa huo, ikiwa ni pamoja na kugawa vyandarua vyenye viuatilifu, kupulizia dawa katika makazi ya watu, kutunza mazingira kote nchini  na kupulizia viuatilifu katika maji yaliyotuama katika baadhi ya maeneo Kanda ya.Ziwa

.

Hawa Ghasia awataka vijana kuchangamkia fursa katika miradi ya Gesi
Magazeti ya Tanzania leo Agosti 24, 2017