Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Ramadhan Manara amesikitishwa na maamuzi ya Uongozi wa Simba SC kumfuta kazi Kocha kutoka nchini Hispania Franco Pablo Martin.

Manara ameonesha masikitiko hayo kupitia ujumbe aliouandika kwenye kurasa zake za mitandao ya Kijamii saa chache baada ya Simba SC kuthibitisha kuachana na Pablo.

Mbali na Kusikitishwa huko, Manara ameipiga kijembe Simba SC kwa kudai ndani ya klabu hiyo kuna mgogoro isiyoisha, huku ikikosa uongozi imara.

Manara ameandika: “Kocha Bora mwenye nidhamu kubwa na mapenzi mazito na football pamoja na Wachezaji wake anaondoka nchini.

Pamoja na kufanya kazi katika Mazingiza magumu ya kukosa Proper Management iliyogubikwa na Migogoro isiyoisha, Jamaa aliiwezesha Club yake kufika Robo fainali ya Shirikisho.

Binafsi ntammiss kwa uungwana wake na ucheshi wake.

Kila la kheri Rafiki yangu Pablo, Kwa msimu huu tu wewe ni Kocha wa pili kufukuzwa na naamini hadi msimu uishe tutasikia mengi”

Kocha Pablo aliajiriwa Simba SC mwishoni mwa mwaka 2021 akichukua nafasi ya Kocha Didier Gomes aliyefukuzwa baada ya kikosi cha klabu hiyo kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Waziri Mkuu awapa maagizo TAMISEMI
Edo Kumwembe: Viongozi Simba SC wanapambana kuivunja timu yao