Mwenyekiti wa Kamati ya wabunge wa Conservative inayohusika na uchaguzi wa viongozi, Grahma Brady amesema kinyang’anyiro cha kumchagua mrithi wa Truss kitafanyika Oktoba 28.

Chama hicho kitapaswa kumchagua kiongozi mpya kabla ya taarifa ya fedha kuwasilishwa mwishoni mwa mwezi huu (Oktoba), huku miongoni mwa majina yanayotajwa kuwania nafasi hiyo yakiwa ni pamoja na Rishi Sunak na mtangulizi wa Truss, Boris Johnson.

Gazeti la The Times, limeripoti kwamba Johnson anakusudia kujiunga katika kinyanganyiro hicho akiamini kwamba kupambania maslahi ya taifa.

Rishi Sunak na Liz Truss: Picha: Hannah McKay/ Reuters.

Hata hivyo, tayari wafuasi wake wameanzisha kampeni ya kutaka kurejeshwa kwa Boris, huku wakosoaji wakiitaja hatua hiyo kama “tusi” kwa waingereza.

Awali, Mbunge, Brendan Clarke-Smith amesema kwamba Waziri Mkuu ajaye wa Uingereza anahitaji “mamlaka” kutoka kwa wapiga kura na wanachama, na kumpigia upatu Johnson kama mwanasiasa aliye na vigezo vyote.

Liz Truss, aLItangaza kujiuzulu baada ya wiki kadhaa za ukosoaji kutoka kwa wapinzani wake na wanachama wake cha Conservative, akiungana na wateule wake wawili wakuu katika baraza la mawaziri ambao nao wameachia ngazi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.

Cedric Kaze aichimba mkwara Simba SC
Noela Luhala: Tutapambana hadi tone la mwisho