Polisi nchini Kenya, iliwabidu  kutumia  gesi ya kutoa machozi kutawanya mkusanyiko wa wafuasi wa upinzani wakati wakiandamana  kupinga ongezeko la kodi.

Kiongozi wa upinzani wa Azimio la Umoja, Raila Odinga ndiye aliyeitisha maandamano kupinga ongezeko la kodi lililowekwa, katika kipindi ambacho watu wengi wanataabika na bei kubwa za bidhaa muhimu.

Hata hivyo, Mahakama Kuu ya Kenya iliamuru ongezeko la kodi liahirishwe lakini Serikali ikaongeza bei ya mafuta ambayo imepelekea uwepo wa changamoto nyingine.

Aidha, inaarifiwa kuwa Polisi waliwakamata wafuasi kadhaa wa upinzani katika mji mkuu na magharibi mwa Kenya, ambao walijitokeza kushiriki maandamano hayo.

Uhimizaji matumizi Kiswahili uendane na vitendo
Rekodi GGML zamkosha Katibu Mkuu Wizara ya Madini