Maafisa wa usalama wa Madagascar wanadaiwa kuwafyatulia gesi ya kutoa machozi Wagombea wa upinzani waliokuwa wakiongoza maandamano katika mji mkuu wa Antananarivo wakiwatuhumu kuwa hayakuwa halali.

Hatua hiyo, inadaiwa inatokana na mivutano ya kisiasa inayongezeka kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Novemba ambapo Wagombea 11 kati ya 13 wa kiti cha rais walitoa wito kwa wafuasi wao kuandamana kupinga mapinduzi ya kitaasisi yanayo mpendelea rais aliyeko madarakani Andry Rajoelina.

Wagombea wa upinzani waliokuwa wakiongoza maandamano katika mji mkuu wa Antananarivo.

Katika tukio hilo, Rais wa zamani wa Taifa hilo na kiongozi Mkuu wa upinzani, Marc Ravalomanana, ambaye alikuwa ni miongoni mwa waandamanaji waliojitokeza kushiriki, aliondolewa na kupelekwa eneo salama na walinzi wake.

Hata hivyo, Wananchi wa Madagascar ambayo ni moja kati ya nchi maskini zaidi duniani licha ya kuwa na maliasili nyingi, wanatarajia kupiga kura ya kumchagua Rais Novemba 9, 2023.

WHO yaridhia chanjo ya pili ugonjwa wa Malaria
Sikoseli: Waziri Ummy azipa agizo Hospitali za Halmashauri