Nigeria imesimamisha mtihani wa kitaifa unaoendelea kwa wanafunzi
wa mwaka wa mwisho katika shule za sekondari kufuatia mapigano
makali yanayoendelea baina ya waandamanaji dhidi ya polisi na
vikosi vya usalama nchini humo.

Baraza la Mitihani la Taifa nchini humo (NECO) limesema uamuzi
wa kusimamisha mitihani hiyo umetokana na amri ya kutotoka nje
iliyowekwa na baadhi ya magavana wa majimbo.

Maeneo kadhaa katika jiji la Lagos yameathiriwa na machafuko hayo
ikiwemo Kituo cha kibiashara cha Lagos, majengo kuteketezwa, vituo
vya ununuzi kuporwa, magereza kushambuliwa pamoja waandamanaji na kupigwa risasi.

NECO imewaamuru wasimamizi wa mitihani kurudi kwenye vituo
vyao na kusubiri maagizo zaidi.

Afisa wa Baraza la Mitihani amesema mitihani hiyo itaanza tena
katikati ya Novemba.

Jana Alhamisi, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari aliwahimiza
waandamanaji kuacha kuandamana na badala yake washirikiane na
serikali “katika kutafuta suluhisho”.

Afariki kwa kula makande na chai.
Walichosema Kinana, Lowassa kuhusu Magufuli