Shirika la Reli la Kenya KRC, limetangaza kusimamisha huduma zote za treni za abiria kufuatia maandamano yaliyoitishwa na Muungano wa Azimio la Umoja ambao umekuwa ukiilalamikia Serikali juu ya uwepo wa hali ngumu ya maisha na upandaji wa gharama za bidhaa muhimu.

KRC imetangaza uamuzi huo hii leo Jumatano, Julai 19, 2023, ikisema hatua hiyo ni muendelezo wa tahadhari kutokana na visa vya hivi majuzi ambapo stesheni ziliharibiwa na treni kupigwa mawe na hivyo kuweka maisha ya abiria hatarini.

Taarifa ya KRC imeeleza kuwa, “Shirika limelazimika kuchukua hatua hizi kwa kuwa usalama wa wateja wetu mara tu huduma za kawaida zitakapoanza tena tutatoa taarifa na tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.”

Tayari Serikali nchini humo pia imezifunga Shule za kutwa za msingi na upili katika maeneo ya Nairobi, Mombasa na Kisumu kutokana hofu ya usalama wa Wanafunzi inayotokana na tangazo la maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika hadi siku ya ijumaa Julai 21, 2023.

Chongolo kuielimisha hadhara uendeshaji wa Bandari
Waziri atoweka baada ya kutangaza uchumba, hofu yatanda